Zana ya bure

QR ya Google Maps: mteja anascan, anafika kwako.

Chagua eneo lako kwenye ramani, kisha pakua QR ya kuweka kwenye bango, kadi, stika au mwaliko. Bure, bila kujisajili.

Bofya kwenye ramani au buruta alama kuweka eneo sahihi.
Una link ya Google Maps tayari? Ibandike hapa

Inavyofanya kazi

  1. 1

    Chagua eneo

    Tafuta jina la mahali, tumia eneo ulipo, au bofya kwenye ramani.

  2. 2

    Pakua QR

    Chagua rangi na fremu, pakua PNG kwa mtandao au SVG kwa uchapishaji.

  3. 3

    Mteja anafika

    Akiscan, Google Maps inafunguka ikiwa na njia ya kufika kwako.

Wapi pa kuiweka

Bango na mlango wa dukaKadi za biasharaMialiko ya harusi na shereheMatangazo ya nyumba za kupangishaVipeperushi na menyuOfisi, kliniki na shule

Unataka eneo lako libadilike bila kuchapisha upya?

Kwenye DP Card, QR ni dynamic: ukihamia ofisi mpya, unabadilisha anwani tu, na kila kadi au bango lililochapishwa linaanza kuelekeza huko. Pamoja na namba, WhatsApp na kitufe cha Njia kwenye kadi moja.

Tengeneza DP Card bure

Maswali

Je, ni bure kweli?

Ndiyo. Hakuna kujisajili wala malipo, na QR haina alama yetu. Unaweza kuichapisha mara nyingi upendavyo.

QR hii inaisha muda wake?

Hapana. Inabeba link ya Google Maps moja kwa moja, kwa hiyo inafanya kazi muda wote, hata bila mtandao wetu.

Nikihamisha ofisi, QR inabadilika?

QR ya bure haibadiliki; ungelazimika kuchapisha mpya. Ukitaka eneo libadilike bila kuchapisha upya, tumia DP Card: QR yake ni dynamic, na kitufe cha Njia kinafuata anwani mpya.

Mteja anahitaji app gani?

Kamera ya simu inatosha. Akiscan, Google Maps inafunguka ikiwa na eneo lako, tayari kumwonyesha njia.

Nichapishe kwa ukubwa gani?

Angalau sentimita 2.5 kwa 2.5 kwenye kadi, na sentimita 10 au zaidi kwenye bango linaloonekana kwa mbali. Kwa uchapishaji, pakua SVG.

Mnaweza kunichapishia?

Ndiyo. DP Promotions inachapisha stika, mabango na kadi zenye QR hii. Tuandikie WhatsApp.