Masharti ya matumizi

Masharti haya yanahusu huduma ya DP Card inayotolewa na DP Promotions Limited, Dar es Salaam.

Akaunti

Unawajibika kwa taarifa unazoweka kwenye kadi zako na kwa usalama wa nenosiri lako. Usiweke maudhui ya udanganyifu, yanayovunja sheria au yanayokiuka haki za wengine. Tunaweza kuzima kadi yenye maudhui ya aina hiyo.

Plan na malipo

Plan za kulipia zinalipwa kabla ya kipindi, kwa mwezi au kwa mwaka. Malipo yanathibitishwa baada ya kupokea muamala wa Mixx by Yas au NMB. Kipindi kikiisha bila malipo, kadi zinaendelea kwa siku 7 zaidi. Baada ya hapo akaunti inarudi plan ya Bure, na kadi zinazozidi kikomo zinasimama mpaka utakapolipa. Ukibadilisha plan katikati ya kipindi, thamani ya siku zilizobaki inahamishiwa kwenye plan mpya kama siku za ziada. Unaweza kusimamisha plan isijirudie muda wowote; itaendelea hadi mwisho wa kipindi ulicholipia.

Kurudishiwa pesa

Malipo yaliyothibitishwa hayarudishwi, isipokuwa huduma imeshindwa kufanya kazi kwa sababu yetu. Wasiliana na huduma kwa wateja: +255 713 671 501.

Alika rafiki

Rafiki anayejisajili kwa link yako anapata punguzo la 20% kwenye malipo yake ya kwanza. Malipo hayo yakithibitishwa, unapata siku za bure zenye thamani sawa na pesa aliyolipa, hadi siku 30, kwenye plan yako ya kulipia, au kwenye Pro kama uko kwenye Bure. Rafiki anayejiunga na Bure bila kulipa haleti zawadi. Hadi zawadi 12 kwa mwaka. Zawadi hazibadilishwi kuwa pesa, na malipo yanayofanywa kwa namba ya simu ya aliyealika au akaunti zinazofunguliwa ili kujizawadia mwenyewe hazistahili.

Upatikanaji

Tunajitahidi huduma ipatikane muda wote, lakini inaweza kusimama kwa muda kwa ajili ya matengenezo au kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.