Faragha
Jinsi DP Card inavyotunza taarifa zako.
Tunachokusanya
Taarifa za akaunti yako (jina, email, namba ya simu), maudhui ya kadi zako, na takwimu za kadi kufunguliwa (muda, njia kama QR au NFC, aina ya simu). Hatuhifadhi anwani za IP kama zilivyo; tunahifadhi alama isiyoweza kurudishwa, inayobadilika kila siku, ili kuhesabu wageni.
Wateja wako
Mtu akijaza fomu kwenye kadi yako, taarifa zake zinaonekana kwako peke yako. Hatuziuzi wala kumpa mtu mwingine.
Ujumbe tunaokutumia
Tunatumia email na WhatsApp kukutumia ankara, vikumbusho vya malipo na taarifa za akaunti. Unaweza kuzima email au WhatsApp kwenye ukurasa wa Akaunti.
Vidakuzi (cookies)
Tunatumia vidakuzi vitatu tu, vyote ni vya lazima ili huduma ifanye kazi: dpc_sid kukuweka ndani ya akaunti (kinaisha ukitoka, au baada ya siku 30 bila kutumia), dpc_lang kukumbuka lugha uliyochagua (mwaka 1), na kidakuzi cha muda cha dakika 10 unapoingia kwa Google. Hatutumii vidakuzi vya matangazo wala vya kufuatilia, na hatuweki Google Analytics wala Facebook Pixel kwenye DP Card. Kwa sababu hiyo hatukuombi ruhusa ya vidakuzi.
Timu na Alika rafiki
Ukimwalika mtu kwenye timu yako, anaona na kuhariri kadi za akaunti yako, lakini haoni bili. Rafiki akijisajili kwa link yako, unaona jina lake la kwanza na kama amelipa, si taarifa nyingine.
Mawasiliano
Maswali kuhusu faragha: sales@dppromotions.co.tz, +255 711 800 400 / +255 673 800 400.