DP Card

Kadi yako ya biashara, kwenye simu ya kila mteja.

Mteja anagusa kadi yako ya NFC au anaelekeza kamera kwenye QR. Namba yako, WhatsApp, email na ramani ya ofisi vinafunguka kwenye simu yake, na anakuhifadhi kwa kubonyeza mara moja.

  • Mteja hahitaji app
  • iPhone na Android
  • Tayari ndani ya dakika 5
<70KB

Ndio uzito wa juu kabisa wa kadi nzima, pamoja na fonti. Inafunguka haraka hata mtandao ukiwa dhaifu, na haimalizi bando la mteja wako.

Unachoweza kutengeneza

Anza na kadi ya kidijitali bure. Ukihitaji, tunakuchapishia kadi za NFC na kuwaandalia wafanyakazi wako wote.

Kadi ya kidijitali

Namba, WhatsApp, email, mitandao na ramani ya ofisi kwenye ukurasa mmoja. Unaishiriki kwa link au QR.

Tengeneza bure

Kadi ya NFC

Kadi ya plastiki yenye chip, inachapishwa na DP kwa rangi na nembo yako. Mteja anaigusa kwa simu, kadi yako inafunguka.

Agiza kadi za NFC

Kadi za wafanyakazi

Kadi kwa kila mfanyakazi chini ya akaunti moja ya kampuni, pamoja na takwimu za kila kadi.

Omba bei ya kampuni

Unachoweza kuweka kwenye kadi

Weka unachohitaji tu. Sehemu ambazo hujajaza hazionekani, na unapanga zilizobaki kwa mfuatano unaotaka.

Mawasiliano yote

Simu mbili, WhatsApp, email na website. Mteja anabonyeza na kukupigia papo hapo.

Njia ya kufika

Kitufe cha Njia kinamfungulia mteja Google Maps hadi mlangoni kwako.

Huduma na bei

Picha, maelezo na bei ya kila huduma, pamoja na kitufe cha kuuliza kwa WhatsApp.

Picha za kazi

Hadi picha 6 za kazi ulizofanya, bidhaa au ofisi yako.

Maoni ya wateja

Maneno ya wateja walioridhika yanampa mteja mpya sababu ya kukuamini.

Nyaraka za PDF

Brosha, menyu, orodha ya bei au wasifu wa kampuni. Mteja anaipakua papo hapo.

Fomu ya mteja

Mteja anaacha jina na namba yake, nawe unapata taarifa kwa email na kwenye dashibodi.

Miadi

Mteja anaomba tarehe na saa ya kukutana, ofisini au kwa simu.

Video, mitandao na saa za kazi

YouTube ya bidhaa yako, kurasa zako za mitandao zenye nembo zake, na siku unazofungua.

Kadi yako hewani kwa hatua tatu

  1. 1

    Jisajili bure

    Kwa email au akaunti ya Google. Hakuna malipo kuanza.

  2. 2

    Jaza na upange

    Weka taarifa zako, chagua mtindo na rangi, panga sehemu kwa mfuatano unaotaka. Kadi inabadilika unapoandika.

  3. 3

    Shiriki

    Kwa QR, link, au kadi ya NFC tunayokuchapishia hapa DP.

Mitindo 20 ya kuchagua.

Chagua mtindo unaoendana na biashara yako na uweke rangi ya kampuni. Unaweza kubadilisha muda wowote bila kuchapisha upya.

Kwa kampuni: kadi kwa kila mfanyakazi, chini ya usimamizi wako.

Wauzaji, madereva, mawakala na mapokezi. Kila mmoja na kadi yake, mwonekano mmoja wa kampuni.

  • Tunawasajili wafanyakazi wote kwa mara moja kutoka faili la Excel.
  • Mfanyakazi akiondoka, unazima kadi yake au unaihamishia kwa anayechukua nafasi yake. QR zilizochapishwa zinaendelea kutumika.
  • Unaona waliofungua kila kadi na wateja walioacha namba zao.
  • Kadi za NFC zenye nembo yenu, tunaziletea ofisini.

Simu: +255 711 800 400 · +255 673 800 400

MfanyakaziWaliofungua, siku 30
Mauzo, Kanda ya Kati184
Mauzo, Arusha131
Mapokezi, Makao Makuu96
Huduma kwa wateja58

Huu ni mfano. Takwimu zako halisi zinaonekana kwenye dashibodi.

Kwa nini DP Card

Imejengwa kwa ajili ya biashara za Tanzania: mitandao ya simu, malipo ya hapa, na huduma ya ana kwa ana.

Link inabadilika, QR inabaki

Ukibadilisha link ya kadi, ya zamani inaendelea kufanya kazi. QR uliyochapisha haiguswi.

Hakuna kikomo cha kufunguliwa

Hata kwenye plan ya Bure, kadi haizimwi kwa sababu imefunguliwa mara nyingi.

Bei kwa shilingi

Lipa kwa Mixx by Yas au NMB na upate ankara rasmi. Hauhitaji kadi ya benki ya kimataifa.

Kiswahili na Kiingereza

Dashibodi na kadi kwa lugha zote mbili. Kila kadi inaweza kuwa na lugha yake.

Kadi za NFC zinatoka kwetu

Hununui kadi tupu mtandaoni wala kupakua app ya kuziandika. Tunachapisha nembo yako, tunaweka link yako kwenye chip na kukuletea.

Unaongea na mtu

Ofisi yetu iko JP Magufuli Rd, Ilala. Unapiga simu au WhatsApp, unajibiwa na mtu wa DP.

Bei wazi, kwa shilingi.

Anza bure. Ongeza kadi biashara yako inapokua. Ukiacha kulipa, kadi yako ya kwanza inaendelea kufanya kazi.

 

Bure

TZS 0
Bila malipo, bila kikomo cha muda
  • Kadi 1
  • Mitindo 3 ya msingi
  • QR, NFC na link ya kudumu
  • Idadi ya waliofungua kadi
Anza bure
 

Lite

TZS 11,999 kwa mwezi
Au TZS 117,999 kwa mwaka, miezi 2 bure
  • Kadi 2
  • Mitindo yote 20, picha, video na fomu ya wateja
  • Takwimu kamili za siku 30
  • Msaada kwa WhatsApp
Chagua Lite
Inayochaguliwa zaidi

Pro

TZS 29,999 kwa mwezi
Au TZS 294,999 kwa mwaka, miezi 2 bure
  • Kadi 5
  • Kila kitu kilicho kwenye Lite
  • Takwimu za siku 90
  • Unahudumiwa kwanza
  • Kadi bila mstari wa DP Card chini
Chagua Pro
 

Business

TZS 70,999 kwa mwezi
Au TZS 707,999 kwa mwaka, miezi 2 bure
  • Domain yako mwenyewecard.kampuniyako.co.tz, bila DP Card kwenye link
  • Kadi 25 za wafanyakazi
  • Takwimu za mwaka mzima
  • Tunawasajili wafanyakazi wote kutoka Excel
  • Mtu maalum wa DP wa kukuhudumia
  • Kadi bila mstari wa DP Card chini
Chagua Business
Kwa makampuni makubwa

Enterprise

TZS 2,899 kwa kadi kwa mwezi
Bei inashuka hadi TZS 1,499 kwa kadi kadri timu inavyokua
KadiBei kwa kadi
1 - 100TZS 2,899
101 - 500TZS 2,199
501+TZS 1,499
  • Domain yako mwenyewecard.kampuniyako.co.tz, bila DP Card kwenye link
  • Kadi kwa kila mfanyakazi, idadi unayochagua
  • Takwimu za mwaka mzima
  • Tunaweka wafanyakazi wote kutoka Excel
  • Mtu maalum wa DP wa kukuhudumia
  • Ankara ya kampuni, malipo ya mwaka au mwezi
Chagua Enterprise

Bei zote zinajumuisha VAT 18%. Malipo kwa Mixx by Yas (Lipa namba 18931680) au NMB. Kila malipo yanapata ankara rasmi. Kadi za NFC zilizochapishwa zinauzwa kando kulingana na idadi.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Mteja wangu anahitaji kupakua app?

Hapana. Kadi inafunguka kwenye browser ya simu yoyote. Akibonyeza Hifadhi, jina lako, namba, email na website vinaingia moja kwa moja kwenye simu yake.

Nikibadilisha namba au kazi, QR niliyochapisha itaendelea kufanya kazi?

Ndiyo. QR na NFC zinaelekeza kwenye link yako ya kudumu. Unabadilisha taarifa kwenye dashibodi, na kila kadi uliyokwisha gawa inaonyesha taarifa mpya.

NFC inafanya kazi kwenye simu zipi?

iPhone XR na zilizofuata, na simu nyingi za Android zenye NFC. Simu isiyo na NFC inatumia QR iliyo upande wa pili wa kadi.

Nalipaje?

Chagua plan kwenye dashibodi, utapata ankara. Lipa kwa Mixx by Yas au NMB, kisha weka namba ya muamala. Tunathibitisha jumatatu hadi jumamosi, saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni na kukutumia ujumbe kwa email na WhatsApp.

Nikichelewa kulipa inakuwaje?

Tunakukumbusha siku 7, 3 na 1 kabla plan haijaisha. Ikiisha, kadi zako zote zinaendelea kwa siku 7 zaidi. Baada ya hapo unarudi plan ya Bure: kadi yako ya kwanza inabaki hewani kwa mtindo wa msingi bila picha, video wala fomu, nyingine zinasimama mpaka utakapolipa.

Naweza kubadilisha link ya kadi yangu?

Ndiyo, muda wowote. Link ya zamani inaendelea kumpeleka mteja kwenye mpya, na QR uliyochapisha haiguswi kwa sababu ina link yake ya kudumu.

Kuna kikomo cha mara kadi inavyofunguliwa?

Hakuna. Kadi inafunguliwa mara nyingi kadiri wateja wanavyotaka, hata kwenye plan ya Bure. Haizimwi kwa sababu imefunguliwa sana.

QR ninayopakua ina alama yenu?

Hapana. QR yako ni safi, kwa PNG ya ukubwa wa kuchapisha au SVG kwa mabango makubwa, kwenye plan zote.

Kadi ya NFC ina ukubwa gani?

Ukubwa wa kadi ya benki, 85.6 kwa 54 mm. Inaingia kwenye pochi na kishikio cha kadi. Upande mmoja tunachapisha nembo yako, mwingine QR kwa simu zisizo na NFC.

Naweza kuweka brosha au menyu kwenye kadi?

Ndiyo. Weka PDF hadi nne, kila moja hadi MB 6. Mteja anaifungua kwenye simu yake bila kuomba utume kwa WhatsApp.

Taarifa zangu ziko salama?

Kila ukurasa unafunguka kwa HTTPS. Nenosiri lako linahifadhiwa kwa njia ambayo hata sisi hatuwezi kulisoma, na namba za wateja walioacha mawasiliano unaziona wewe peke yako.

Namba za wateja walioniachia ni za nani?

Ni zako. Unaziona kwenye dashibodi na kuzipakua kwenye Excel. Hatuuzi wala kumpa mtu yeyote taarifa zako.

Tengeneza kadi yako leo.

Ni bure, na inachukua dakika 5.